#WenyeNchiWananchi
Kura ya maoni ni ulinzi dhidi ya maamuzi ya mabavu. Viongozi wasio na nia njema hawawezi kupitisha mabadiliko ya hatari kirahisi iwapo kuna kura ya maoni #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 17, 2026 at 5:00 AM
Tanzania inahitaji katiba mpya inayotokana na wananchi, inayoheshimu utawala wa sheria, na kutoa mwelekeo wa maendeleo ya Taifa na kulinda haki za wananchi, Katiba ya sasa haitambui haki za kiuchumi wanazostahili pata wananchi #KatibaMpya youtu.be/0zFhUAp2I0Y
HISTORIA YA KATIBA NA NINI MAONI YA WATANZANIA
Katiba ni nyenzo muhimu ya utawala bora, inayotoa msingi wa sheria, haki na majukumu ya raia pamoja na muundo wa dola. Kuna mapungufu makubwa ya haki za binadamu kwenye katiba ya sasa, vyombo vya dola havina uwajiibikaji wowote. Katiba ya Tanzania, ya mwaka 1977, ilitungwa chini ya mfumo wa chama kimoja na haijakidhi mahitaji ya mfumo wa vyama vingi unaotumika leo , Hii ndio sababu CCM wanajiona kama CHAMA kinachomilini nchi, Chama Dola #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
youtu.be
June 21, 2026 at 6:00 AM
MAFUNZO YA KIDIJITALI KWA VIJANA‼️

Mada

1. Uandishi wa Habari wa Kiraia

2. Elimu ya Katiba Mpya

3. Usalama Mtandaoni — Kwa Kundi Maalum
4. Ujenzi wa Harakati

Wahi ujisajili forms.gle/QFAgSsozn8Zd...

Jaza fomu kabla ya Sept 24
Kuanza Sept 28

#WenyeNchiWananchi
September 19, 2026 at 5:08 AM

Uongozi ni dhamana upita baada ya nyakati, lakini Nchi, wannachi na mifumo ya utawala ni suala la wananchi. Hatuwezi kuruhusu misingi ya Taifa letu ibadilike kulingana na matakwa au mihemko ya viongozi wa wakati husika. Katiba ni dira yetu sisi Wananchi kwa manufaa yetu. #WenyeNchiWananchi
August 7, 2026 at 6:40 AM

Uhalali wa kikatiba (constitutional legitimacy) unaharibika pale wananchi wanapoona kuwa mchakato unaratibiwa na vyombo vile vile vinavyotuhumiwa kukiuka misingi ya utawala bora. Wasimamizi huru wanatoa imani kwa umma kuwa mageuzi yanayokusudiwa ni ya dhati. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 31, 2026 at 6:00 AM

Kisheria, kuna kanuni ya "Nemo judex in causa sua" (hakuna mtu anayepaswa kuwa mwamuzi wa kesi yake mwenyewe). Kanuni hii inapaswa kutumika katika mageuzi ya kikatiba; watawala hawawezi kuwa waamuzi wa mipaka ya madaraka yao wenyewe kupitia mchakato wanaouongoza wao. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 29, 2026 at 4:44 AM
Kama mkataba mkuu wa kijamii, Katiba inapaswa kuandikwa kwa wino wa maoni na vipaumbele vya wananchi. Viongozi ni mawakala tu wa kutekeleza mkataba huo; hawana haki ya kisheria au kimaadili kubadilisha kile ambacho umma umeamua. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 28, 2026 at 12:50 AM

Katiba inayodumu na kuheshimiwa ni ile inayomilikiwa kisaikolojia na kivitendo na wananchi. Umiliki huu unapatikana wananchi wanapopewa nafasi kamili, bila shinikizo la kisiasa, kuamua sheria mama wanayoitaka kuongoza maisha yao na vizazi vijavyo. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 25, 2026 at 9:17 AM

Dhana ya mamlaka ya umma (popular sovereignty) inasisitiza kuwa nguvu zote za kiutawala zinatoka kwa wananchi. Hivyo, uamuzi wa mwisho kuhusu muundo na maudhui ya Katiba Mpya unapaswa kubaki mikononi mwa raia wenyewe kupitia michakato huru na ya wazi. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 24, 2026 at 1:06 PM

Katiba Mpya yenye tija inasimama kama kioo cha maridhiano ya kitaifa. Mchakato wake unapaswa kuendeshwa kwa misingi ya haki, uwazi na ujumuishi, na sio utashi wa kisiasa au upendeleo wa viongozi waliopo madarakani. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 23, 2026 at 2:50 PM
Katika misingi ya sheria za kikatiba, uhalali wa mchakato (procedural legitimacy) ni muhimu sawa na yaliyomo kwenye katiba yenyewe. Mchakato unaoendeshwa kama hisani ya viongozi unakosa sifa hii muhimu ya kisheria na kijamii. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 23, 2026 at 3:00 PM

Kuanzia kwa mama lishe, machinga, hadi mkulima wa kijijini—haki ya kujitafutia riziki na kulinda utu wako inasamiwa na Katiba. Ni silaha yetu ya kiuchumi; tusikubali iwekwe kando au kupuuzwa. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 21, 2026 at 4:51 PM

Silaha kubwa ya kupambana na dhuluma, rushwa, na ubadhirifu wa mali za umma nchini Tanzania ni Katiba thabiti. Inampa mwananchi wa kawaida nguvu ya kisheria kuhoji na kuwawajibisha viongozi. Katiba imara, Taifa imara! #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 21, 2026 at 4:50 PM

Katiba imara sio tu karatasi, ni ngao inayomlinda mwananchi wa kawaida dhidi ya uonevu na matumizi mabaya ya madaraka. Kulinda Katiba ni kulinda haki yako ya kuishi, kufanya kazi, na kujieleza kwa uhuru. #KatibaMpya #WenyeNchiWananchi
July 20, 2026 at 9:30 AM